April 21, 2016


Na Saleh Ally, La Coruna
Washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Spain na Azam Sports HD” wamekamilisha ndoto yao ya kushuhudia moja kwa moja mechi ya La Liga kati ya Barcelona waliokuwa wageni wa Derpotivo la Coruna.


Washindi hao wameshuhudia mechi hiyo kwenye Uwanja wao wa Raizor jijini na wageni Barcelona wakashinda mabao 8-0 huku Luis Suarez akitupia manne peke yake lakini Lionel Messi na Neymar kila mmoja akafunga moja na kukamilisha MSN kuwa imefunga.


Mechi hiyo ilikuwa tamu na yenye mvuto na mashabiki hao kutoka Tanzania, mmoja akiwa shabiki wa Simba na mwingine wa Yanga walionyesha furaha yao wazi.

Ilikuwa furaha kuu baada ya wao kushuhudia mechi hiyo lakini kabla walipata nafasi ya kukaa karibu kabisa na wachezaji wa timu zote mbili wakati wakiingia vyumbani, jambo ambalo si rahisi kupatikana hata kwa raia wenyewe wa Hispania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV