April 16, 2016

YANGA YAREJEA KILELENI LIGI KUU BARA




Yanga sasa imefikisha pointi 59 na kuwa kileleni katika Ligi Kuu Bara ikifuatiwa na Simba ambayo ina pointi 57, timu zote hizo zimecheza mechi 24 kila moja, zimesaliwa na mechi 6 kumaliza msimu wa 2015/2016.

MPIRA UMEKWISHA: Dakika 90 na zile za nyongeza zimekamilika, mpira umemalizika kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga imepata ushindi wa bao 1-0.

DAKIKA NNE ZA NYONGEZA


Dakika ya 90
Dakika ya 88, Mtibwa wanapambana kutafuta bao la kusawazisha lakini bado mambo ni magumu.

Dakika ya 85, Mbonde anatoka, anaingia Boniface Maganga.
Dakika ya 84, Busungu anakosa bao la wazi kabisa, anapewa pasi na Tambwe, anabaki yeye na kipa anapiga shuti linatoka nje.
Dakika ya 81, Mbonde anaomba kutoka kutokana na maumivu anayoyasikia.
 
Mbonde

Dakika ya 80, beki wa Mtibwa, Mbonde yupo chini akiwa ameumia, mchezo umesimama kwa muda.
Dakika ya 78, Msuva anakosa bao akiwa yeye na kipa, anapigiwa pasi na Niyonzima, anatuliza kisha shuti lake linadakwa na Said.

Dakika ya 77, Yanga bado anaongoza 1-0, mfungaji akiwa ni Msuva.
Dakika ya 76 Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kaseke anaingia Amiss Tambwe.

Mtibwa nao wanafanya mabadiliko anatoka Kichuya anaingia Vicent Barnabas.
Dakika ya 75, mashabiki wa Yanga wanamzomea kipa wa Mtibwa, Said ambaye baada ya kudaka mpira anaupiga kwa haraka tofauti na mwanzoni ambapo alionekana kuchelewesha kuuanza mpira pindi alipodaka.

Dakika ya 73, Yanga wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia, inaokolewa na mabeki wa Mtibwa.
 Dakika ya 69, Yanga bado wanaendelea kulishambulia zaidi lango la Mtibwa lakini wanashindwa kutumia nafasi wanazopata.

Dakika ya 65, Ngoma anakosa bao la wazi baada ya Andrew Vicent wa Mtibwa kukosea pasi na kumpasia Ngoma ambaye shuti lake linakosa mwelekeo.
Dakika ya 62, Juma Abdul anapiga shuti kali linatoka hatua chache kutoka nje ya lango la Mtibwa, inakuwa kona, Yanga wanpiga kona lakini haina madhara.

Dakika ya 58, Yanga wanafanya shambulizi la nguvu kwa counter attack baada ya Mtibwa kushindwa kuitumia vizuri kona waliyoipata, Msuva anashindwa kutumia nafasi ambayo anaipata baada ya kumtoka kipa wa Mtibwa lakini pasi yake inanaswa na mabeki wa Mtibwa ambao wanaondoa hatari.
Dk 57 Mtibwa wanagongeana vizuri lakini Kichuya anabutuaaaaaa

Dakika ya 52, Mtibwa wanafanya mabadiliko, anatoka Ibrahim Rajab wa Mtibwa anaingia Henry Joseph.
Dakika ya 46, Niyonzima anapiga faulo kwa kupasia Msuva, ambaye anatuliza kisha kupiga shuti kali ambalo linamshinda kipa wa Mtibwa, Said Mohamed. Yanga moja, Mtibwa hawajapata kitu.

GOOOOOO DK 46 Msuva anaifungia Yanga bao kwa shuti kali nje ya 18




Dakika ya 46, Yanga wanapata faulo.
Dk 46 Yanga wanaanza kwa kushambulia wakionekana wamepania kupata bao

MAPUMZIKO
Mechi ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar imeshaanza kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, mchezo huo wa Ligi Kuu Bara, umeanza na sasa ni dakika ya 28 matokeo bado ni 0-0.

Benchi la Yanga likiongozwa na Kocha Mkuu Hans Van Pluijm (kulia).

Kutokana na mvua ambayo imenyesha jijini Dar es Salaam, uwanja umekuwa na maji mengi na kusababisha baadhi ya wachezaji kuteleza na kupoteza kontroo.


Bossou
Kocha Pluijm, leo amefanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambapo Bossou anacheza namba sita akiwa kiungo mkabaji tofauti na ilivyozoeleka ambapo amekuwa akicheza beki wa kati, wakati Amiss Tambwe leo yupo benchi yawezekana kutokana na kiwango chake kuonekana kuwa katika hali ambayo siyo nzuri katika siku za hivi karibuni.

Kikosi cha Yanga:
1. Deogratius Munishi ‘Dida’
2. Juma Abdul
3. Oscar Joshua
4. Kelvin Yondan
5. Nadir Haroub ‘Cannavaro’
6. Vicent Bossou
7. Simon Msuva
8. Thaban Kamusoko
9. Donald Ngoma
10. Haruna Niyonzima
11. Deus Kaseke

Mchezo bado ni mkali na mashambulizi ni ya kupokezana kwa timu zote.

Kikosi cha Mtibwa Sugar
1. Said Mohammed
2. Ally Shomari
3. Majaliwa Shabaan
4. Andrew Vicent
5. Salim Mbonde
6. Shaban Nditi
7. Shiza Kichuya
8. Muzamiru Yassin
9. Seleman Rajabu
10. Ibrahim Rajab
11. Kelvin Friday


Dakika ya 32, Seleman Rajab wa Mtibwa anapewa kadi ya njano kutokana na kumchezea faulo mbaya Kamusoko, baada ya faulo hiyo Kamusoko alitoka nje ya uwanja kutibiwa lakini alirejea baada ya muda mfupi.
Dakika ya 35, Niyonzima anakosa bao la wazi baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa wa Mtibwa.

Yanga wanaonekana kulishambulia zaidi lango la Mtibwa lakini bado wameshindwa kuonyesha umakini wanapofika langoni.
Dakika ya 45, zimeongezwa dakika 2 za nyongeza. 
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimekamilika, timu zote zimeingia vyumbani kupumzika.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic