April 12, 2016



Dakika chache tu baada ya ratiba ya Kombe la Shirikisho kupangwa, Yanga na Azam FC zimetaka mechi zao za nusu fainali kusogezwa mbele.

Azam FC inatakiwa iwe mgeni wa Mwadui FC Aprili 24 na Yanga iwe mgeni wa Coastal Aprili 24 pia. Lakini zinakabiliwa na michuano ya kimataifa.

Azam FC itasafiri kwenda Tunisia kuwavaa Esperance katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho na Yanga itakuwa Cairo kuwavaa Misri dhidi ya Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.



Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema ni vema kama ratiba itasogezwa mbele kwa kuwa watakuwa wanatokea Tunisia ambako watasafiri kwa zaidi ya saa 8. 

“Hatuwezi kurudi baada ya siku moja tucheze, itakuwa ni safari ndefu. Hivyo TFF waliangalie hilo,” alisema Kawemba.

Naye Msemaji wa Yanga, Jerry Muro alisema anaungana na Azam FC katika hilo.

“Waliangalie, wajue tuna majukumu ya kimataifa na waone urefu wa safari yetu,” alisema Muro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic