BAWAZIRI AKIHOJIWA NA BARUAN MUHUZA WA AZAM TV |
Kaimu Katibu Mkuu wa Coastal Union, Salim Bawaziri amesema wana kila sababu ya kubeba Kombe la FA.
Coastal Union imepangwa na Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho ambayo itapigwa Aprili 24 mjini Tanga.
“Watu watofautishe Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara. Kwenye ligi hatufanyi vizuri lakini Shirikisho hakuna mjadala, tunachukua.
“Hao Yanga wanajua kwamba wanaanzia Mkwakwani ambako ni machinjioni, hakuna mjadala watakwisha pale,” alitamba.
Coastal imevuka baada ya kuiangusha Simba na kuweka rekodi ya kuwa timu iliyozifunga Yanga, Azam FC na Simba ndani ya dakika 90 kwenye Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment