April 5, 2016

Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameanza maandalizi yao kwa ajili ya kuivaa Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga iko mjini Pemba ambako inafanya maandalizi kwa ajili ya mechi yao ya Jumamosi.

Kocha Hans van der Pluijm amesema watafanya maandalizi yao kwa umakini mkubwa.

“Tunahitaji muda wa kujipanga, tuna mengi ya kujifunza na kuangalia wapinzani wetu wana nini.

“Tulianza mapema, lakini huku pia tuna nafasi ya kuendelea kufanya maandalizi kwa utulivu zaidi,” alisema.


Kabla ya kwenda Pemba, Yanga ilianza maandalizi yake jijini Dar es Salaam na ilikuwa inajifua kwenye Uwanja wa Gymkhana.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV