April 25, 2016


Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo atakuwa fiti kesho katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City.

Madrid wako ugenini na leo wamefanya mazoezi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester.

Zidane amesema Ronaldo yuko tayari kwa ajili ya mechi hiyo, maana yake ataanza katika mchezo huo.

Kulikuwa na hofu Ronaldo kukosekana baada ya kukosa mechi iliyopita ya La Liga.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV