May 10, 2016


Amissi Tambwe amefunga boa lake la 21 leo, akimfunga kipa mkongwe nchini Juma Kaseja.

Tambwe raia wa Burundi amefunga bao hilo likiwa ni la pili kwa Yanga katika mechi ambayo wameshinda kwa mabai 2-0 dhidi ya Mbeya City.

Bao lake hilo la 21 msimu huu ni gumzo, sasa anamuacha mshambuliaji Mganda wa Simba, Amissi Kiiza kwa mabao mawili kwa kuwa ana 19.

Tambwe amefunga bao hilo akiwa umbali wa takribani mita 23, ilikuwa kama anatuliza lakini tayari alijua Kaseja alikuwa amesogea mbele, akaachia shuti lililojaa wavuni moja kwa moja.


1 COMMENTS:

  1. Hahahahahahah!Mayanja alisema Tambwe hawezi kumpita Kiiza kwa ufungaji,tusubiri Simba atakavyomgaragaza majimaji leo halafu tutatoa tathmini.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV