Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga amefurahia kusikia mechi yao dhidi ya Ndanda FC itachezwa Dar es Salaam badala ya Mtwara.
Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi amesema anaona ni jambo zuri kwa kuwa Yanga inapaswa kujiandaa kwa ajili ya mechi yao ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Esperanca ya Angola.
“Tuna safari ndefu na ngumu kuhakikisha tunaulinda ushindi wetu wa mabao mawili. Angalau kutokwenda Mtwara kutatusaidia kupunguza uchovu kidogo.
“Tutakapofika mji mkubwa wa Luanda, bado tunatakiwa kwenda mji mwingine. Hivyo kucheza Dar es Salaam, kutakuwa na ahueni angalau,” alisema.
Ndanda na Yanga zimekubaliana mechi hiyo kupigwa Dar es Salaam badala ya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
0 COMMENTS:
Post a Comment