May 3, 2016


Bayern Munich imeng’olewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kushinda kwa mabao 2-1 ikiwa nyumbani Munich, Ujerumani.

Atletico Madrid imesonga kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa bao la ugenini baada ya ushindi wa bao 1-0 ikiwa nyumbani Madrid.

Kusonga mbele kwa Atletico Madrid, maana yake Kocha Pep Guardiola ambaye anaondoka kwenda kujiunga na Manchester City, ameshindwa kutimiza ndoto yake ya kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Bayern.

Mechi ilikuwa ngumu na tamu kuangalia na wenyeji walianza kupata bao katika dakika ya 31 kupitia Xabi Alonso.

Lakini Antoine Griezmann akaisawazishia Atletico kabla ya Robert Lewandowski kuongeza la pili.

Kila timu ilikosa penalti wakianza Bayern kupitia Thomas Muller na upande wa Atletico, Fernando Torres naye akakosa, makipa wa timu zote wakiwa mashujaa kwa kuzipangua.

Atletico Madrid inasubiri mshindi kati ya Real Madrid dhidi ya Manchester City katika mechi itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV