May 3, 2016


Kiungo wa Simba, Ibrahim Ajib amejiunga na kikosi cha Simba na kuanza mazoezi rasmi.

Ajib alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria uliomuweka nje ya kikosi hicho.

Meneja Abbas Gazza amesema Ajib ameungana na wenzake na kufanya nao mazoezi.

“Ndiyo Ajib amerejea, amefanya mazoezi na wenzake,” alisema Abbas.

Simba iko katika maandalizi ya mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC itakayochezwa Jumapili.

Hata hivyo, kiungo huyo amekuwa akizidi kuporomoka kila siku zinavyosonga mbele.

Ajib alikuwa tegemeo katika uchezeshaji na hatari kwa mabeki wa timu pinzani. Lakini kila ligi inavyosonga ukingoni, amekuwa akionekana kuporomoka kiwango chake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV