May 7, 2016


Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu amemuomba kocha wake, Hans van Der Pluijm ampe nafasi ya Donald Ngoma katika mchezo wa leo dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Yanga inacheza mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Esperanca baada ya kutolewa na Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa hivi karibuni.

Wachezaji Donald Ngoma na Thabani Kamusoko hawatakuwepo katika mchezo huo wa leo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano walizopata katika michezo iliyopita. 

Kutokana na hali hiyo, Pluijm analazimika kumchezesha ama Busungu au Anthony Matheo mmoja wao acheze na Amissi Tambwe katika nafasi ya ushambuliaji ambayo awali Ngoma alikuwa anacheza.

Busungu amesema: “Nikipewa nafasi ya Ngoma katika mchezo huu, nina uhakika wa kuiwezesha Yanga kupata ushindi.


“Nipo vizuri kabisa, namuomba kocha anipe nafasi ya Ngoma naahidi nitafanya vizuri kama anavyofanya Ngoma kwa manufaa ya Yanga.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV