May 25, 2016



Ukizungumzia wachezaji wanaong’ara zaidi duniani kwa sasa au wanaoongoza kwa kuchukua tuzo kubwa duniani ni wale wanaotokea Amerika Kusini.

Mfano ni nchi za Brazil, Argentina, Chile, Uruguay na nyinginezo. Huko utawakuta watu kama akina Lionel Messi, Neymar, Luis Suarez, Alexis Sanchez na wengine wengine wanaotamba katika ligi kubwa za Ulaya.

Inapofikia michuano ya bara la Amerika Kusini na ukanda wa kati, maana yake unawakutanisha mawgiji, hiyo mi michuano ya Copa America.

Copa America ndiyo michuano mikongwe zaidi ya mabara duniani. Ilianza mwaka 1916. Awali ilifanyika kila mwisho wa mwaka na baadae ikajitangaza na kuwa sababu ya uandaaji wa kombe la dunia 1930.

Michuano hii inatarajia kuanza Juni 4 hadi 27, uhondo ambao utarushwa moja kwa moja na StarTime, itakuwa ni kazi kubwa kwa wapenda soka kukubali kuikosa.

Inafanyika nchini America, ikishirikisha timu 16 kwa kujumlisha mashirikisho mawili ya mabara ya Amerika Kusini na Kaskazini huku kukiwa na miji 10 ambayo mechi zake zitachezwa.

Michuano hii inajitosheleza na imekuwa ikizaa matunda kwa timu za taifa za ukanda huu, kwa mfano Uruguay walikua vizuri sana katika kombe la dunia la 2010 Afrika Kusini wakati Colombia wakitesa katika fainali zilizopita. Timu hizi kutoka ukanda huu ni nadra sana kutolewa hatua za awali za michuano ya kombe la dunia.

Makundi manne ya Copa America haya hapa:
Kundi A:
USA, COLOMBIA, PARAGUAY NA COSTA RICA
Kundi B:
BRAZIL, PERU, HAITI na EQUIDOR
Kundi C:
MEXICO, URUGUAY, JAMAICA na VENEZUELA
kundi D
ARGENTINA, CHILE, PANAMA na BOLIVIA
Michuano hii itarusha na StarTimes pekee kupitia channel za michezo


#CopaAmericaOnStarTimes #Exclusive
Download app ya StarTimes kujishindia zawadi www.startimes.com


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic