Na George Mganga
Licha ya kusikitishwa na maamuzi yaa aliyekuwa mchezaji wao, Mzimbambwe, Donald Ngoma kuondoka na kutimkia Azam FC kisha kusaini mkataba wa mwaka mmoja, uongozi Yanga umesema ulipanga kumpa mapumziko ya mwaka mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Maadili wa klabu hiyo, Hussein Nyika, ameeleza kuwa Yanga ilipanga kumpa mapumziko ya mwaka mmoja Ngoma ili aweze kutibiwa vizuri na hatimaye aweze kurejea Uwanjani.
Nyika ameeleza uongozi ulijipanga kwa ajili ya kufanya hivyo ili kumpa muda mzuri Ngoma wa kuweza kupata matibabu akiwa amepumzika ili hata akili yake kisaikolojia iweze kukaa vizuri.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya mchezaji huyo aliyekuwa kwenye matibabu kuandamwa na majeraha ndani ya msimu mzima wa 2017/18 kusajiliwa na Azam FC.
Tayari Ngoma ameshaijiunga na Azam na amesaini mkataba wa mwaka mmoja na wiki ijayo atapelekwa Afrika Kusini kufanyiwa vipimo vya afya kisha matibabu endapo vipimo vitaonesha ana matatizo kiafya.
Jambo muhimu hapa ni kitendo cha Azam kuchukua jukumu la kumtibia Ngoma ili aweze kutumikia timu. Baada ya matibabuanaweza kuwa fiti akatoa mchango mkubwa kwa timu lakini pia anaweza asiwe fiti. Muhimu hapa ni lie dhamira nzuri ya kumtibia kwanza. Ni jambo la kupongezwa
ReplyDeleteMapumziko ya mwaka mmoja?????cjawahi ckia
ReplyDeleteHivi ukiwa mgonjwa ukaamua kulala tu bila matibabu au dawa je utapona?Yanga wanapaswa kuwa wanatoa matibabu wachezaji wanapoumia
ReplyDeleteHivi ukiwa mgonjwa ukaamua kulala tu bila matibabu au dawa je utapona?Yanga wanapaswa kuwa wanatoa matibabu wachezaji wanapoumia
ReplyDeleteHivi ukiwa mgonjwa ukaamua kulala tu bila matibabu au dawa je utapona?Yanga wanapaswa kuwa wanatoa matibabu wachezaji wanapoumia
ReplyDeleteWakampe basi Tambwe mapumziko ya mwaka mmoja
ReplyDeleteyanga inapita katika kipindi kigumu hivyo tungejitahidi Kuwapa moyo badala ya kuwashambulia kwa kila tendo walifanyalo
ReplyDeleteKauli tata za Yanga ndiyo zinasababisha maswali hayo
ReplyDeleteViongozi waache kujitetea na inabidi waongoze mpira kiuweledi waache ujanja ujanja,Mchezaji kaumia akiwa kazini inabidi apate tiba sahihi,lakini walichofanya inam demotivate mwajiriwa,Na si wamesema walikubaliana kuvunja mkataba sasa mbona maneno mengi,Jus move on na usajili mwingine makini tena kwa ukata wetu mi naona tusajili wachezaji wa ndani tu wenye viwango na ma pro watatu tu
ReplyDelete