May 23, 2018


Taarifa zilizo chini ya kapeti zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Simba umepanga kuachana na Kocha wake Mfaransa, Pierre Lechantre huku nafasi yake ikichukuliwa na Msaidizi, Mrundi, Masoud Djuma.

Simba wamefikia hatua ya kufanya maamuzi hayo ikiwa timu yao inajiandaa kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayotarajia kuanza mwezi Juni nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka kwa mabingwa huo wapya wa ligi kwa msimu wa 2017/18 zinaeleza kuwa Simba haijaridhishwa na kiwango cha Mfaransa huyo anayepokea mshahara mkubwa kuliko Makocha wote wa Ligi Kuu Bara.

Kutokana na hali hiyo uongozi umedhamiria kumpa timu Mrundi, Masoud Djuma huku ikiwa haijaelewa kama atakuwa Kocha Mkuu au ataletwa mwingine kuchukua mikoba ya Mfaransa huyo.

Hivi karibuni taarifa zilieleza kuwa Lechantre amekuwa miongoni mwa makocha waliotuma barua kwenda Cameroon akiomba nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya nchini humo, hivyo endapo kama atafanikiwa kuipata itakuwa ni safari yake ya kuiacha Simba.

Mfaransa huyo alikuja Simba na kusaini mkataba wa miezi sita ambao unamalizika ndani ya mwezi ujao.

Lechantre alikuja Simba kuchukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog, aliyefukuzwa mapema baada ya timu kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka jana na Green Warriors kwa bao 1-0.

4 COMMENTS:

  1. Alikuwa na jina kubwa kutokana na CV lakini bila ya ueexo kuifanya timu yrnye kama ile Almasri kutokana na nyota bora kulilo timu xote ambapo Simba ingeweza kumaliza ligi na pointi zisizopunguw thamanini, lakini ilikosa kasi na iliwexa kupata ubingwa kutokana na ubora wa wachezaji na wala si uwezo wa mwalimu

    ReplyDelete
  2. Yamekuwa hayo tena? Duuuuuh!!!!!!

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  3. Masoud Djuma ni kocha mzuri hakuna ubishi lakini hawezi kuvaa viautu vya mfaransa hata siku moja. Mfaransa ana kandarasi ya miezi sita na simba. Miezi sita sio mkataba wa kumfanya kocha mwenye heshima zake ajisikie yupo kazini na kuwa mtulivu katika kazi yake. Nnaamini kabisa mfaransa yupo kiutalii zaidi kuliko kazini. Sababu zinaweza kuwa nyingi ya Simba kuweza kuachana na mfaransa lakini kikubwa zaidi ni gharama za kocha huyo lakini kwa sarakasi za Simba na Yanga wala usije ukashangaa kusikia Lwandamina kuwa kocha mpya wa Simba.

    ReplyDelete
  4. Lwandamila kuja Simba hapana. Simba inahitaji kocha wa daraja la juu zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic