May 11, 2016


Straika wa Yanga, Malimi Busungu bado anauguza majeraha mbavu aliyopata katika mchezo dhidi ya Sagrada Esperanca, ametakiwa kutocheka kwa nguvu wala kuzungumza muda mrefu ili aweze kupona haraka.

Busungu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Barracks iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam baada ya kuumia uwanjani Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola.

Akicheza nafasi ya Donald Ngoma aliyekuwa akitumikia adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano, Busungu aligongana na kipa wa Sagrada Esperanca, Yuri Tavazes na kuvunjika mbavu mbili ndogo za upande wa kulia.

Akizungumza na Championi Jumatano, Busungu alisema: “Naendelea vizuri ila madaktari wamenizuia kucheka kwa nguvu wala kuzungumza muda mrefu ili niweze kupona haraka.

“Madaktari waliniambia hivyo kwa sababu nilipokuwa nikicheka au kuzungumza muda mrefu nilikuwa nahisi maumivu makali sehemu niliyoumia.

“Hata hivyo namshukuru Mungu hivi sasa naendelea vizuri, kama mambo yasipobadilika basi Ijumaa (keshokutwa) naweza kutoka hospitali,” alisema Busungu.


1 COMMENTS:

  1. Pole sana jembe,TUNAKUOMBEA UPONE HARAKA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic