May 2, 2016

HII ILIKUWA MECHI DHIDI YA COASTAL UNION...

Mabeki wa Toto African waliamua kutembeza kiatu ili kupunguza kasi ya mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma. Katika mechi hiyo, Mzimbabwe huyo alifanyiwa madhambi mara 11.

Yanga ilishinda 2-1 kwa taabu lakini Toto walifanikiwa kumdhibiti Ngoma kwa rafu ambazo kuna baadhi zilionekana lakini nyingine hazikuonwa na mwamuzi.

Katika mchezo huo ambao Ngoma alikuwa akikabwa na Hassan Khatibu pamoja na Carlos Protus, alionekana kupata shida kila alipopata mpira kwani mabeki hao walikuwa wakimkaba kwa pamoja, jambo lililosababisha beki Protus kupewa kadi ya njano baada ya kuonekana kumchezea vibaya Ngoma.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Ngoma alisema ni kweli amechezewa rafu nyingi lakini hiyo yote ilitokana na kuwa msumbufu.

 “Nilikuwa nikiwasumbua sana, ndiyo maana walikuwa wakishindwa kunimudu na kuamua kunichezea vibaya lakini namshukuru Mungu sijaumia, niko fiti,” alisema.

Ngoma aliongeza kuwa, mabeki wengi wa timu zinazocheza Ligi Kuu Bara, wamekuwa wakimchezea vibaya.
 “Nimegundua kuwa mabeki wengi wa ligi kuu hawafanyi mazoezi ya kutosha, sasa kila tunapokutana nikiwachenga kidogo wananiangusha, mfano ni beki wa Simba, Abdi Banda, alipata kadi nyekundu baada ya kuona nimemzidi ujanja, hivyo nachezewa vibaya kutokana na mabeki kutokuwa na uwezo wa kunikaba,” alisema Ngoma.

Kwa upande wake beki wa Toto, Carlos Protus, alisema Ngoma hakabiki, ndiyo maana walitafuta mbinu mbadala ya kumdhibiti ili asifunge. “Ngoma ni msumbufu sana, ndiyo maana tulimkaba kwa zamu na tukafanikiwa,” alisema.

Kwa upande wake, Khatibu alisema Ngoma ndiye aliyekuwa mchezaji msumbufu katika mchezo huo licha ya kutofunga bao.


1 COMMENTS:

  1. Wale wa kusema Yanga inabebwa someni taarifa hiyo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic