May 13, 2016


Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limemtangaza katibu wake mkuu mpya, safari hii akiwa ni mwanamama tena kwa mara ya kwanza.

Rais wa Fifa, Gianni Infantino, amemtangaza Fatma Samoura aria wa Senegal.

Fatma anakuwa mwanamke wa kwanza duniani kushika nafasi ya juu katika mchezo wa soka.

Mwanamama huyo anatarajia kuanza kazi yake rasmi mwezi ujao, na Infantino amesema hakukuwa na shinikizo wala ushawishi badala yake kazi nzuri ya Fatma.


Kwa sasa, Fatma ni mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) akiwa nchini Nigeria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV