Kocha Jonas Luis ametua nchini tayari kufanya mazungumzo na uongozi wa Azam FC ili kuchukua nafasi ya Stewart Hall.
Luis raia wa Hispania, anayeinoa Derpotivo Tenerife inayoshiriki daraja la kwanza Hispania tayari yuko nchini na alipolekewa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba.
Kocha huyo ameongozana na msaidizi wake Zebensul Harnandez pia raia wa Hispania.
Taarifa zinasema makocha hao watapata nafasi ya kukiona kikosi cha Azam FC kitakachokuwa kikipambana na African Sports katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Hall raia wa Uingereza, tayari alishaeleza kuwa ataondoka Azam FC baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Bara.
Hata hivyo, kocha huyo atabaki na timu hiyo hadi atakapocheza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment