May 9, 2016


Kocha wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, amewataja wachezaji anaowahitaji katika kikosi chake cha msimu ujao ili Simba iondokane na kadhia ya kukosa mataji kila msimu.

Simba ambayo mpaka sasa imepoteza matumaini ya kutwaa taji lolote msimu huu, msimu ukimalizika watakuwa wanatimiza mwaka wa nne mfululizo bila ya taji la Ligi Kuu Bara huku msimu wao wa mwisho kubeba taji hilo ukiwa ni wa 2011/12.

 Mayanja alisema wachezaji wazoefu ndiyo wanapaswa kusajiliwa na Simba katika kipindi kijacho cha usajili ili msimu ukianza waweze kuendana na kasi ya ligi.

“Simba inatakiwa kusajili wachezaji wengi wazoefu waliokomaa tayari na wanajua kuwa soka ndiyo kazi yao kama ilivyo kwa Yanga na Azam.

“Hali hiyo itatusaidia sana kuendana na kasi ya ligi na itatusaidia kutimiza malengo yetu ambayo tunahitaji kuyatimiza ikiwa ni pamoja na kutwaa mataji mengi,” alisema Mayanja.


2 COMMENTS:

  1. Yeye mwenyewe tayari kashaonyeshewa taa ya kijani!

    ReplyDelete
  2. kama kuna kitu nimechoka ni siasa za simba afadhal za yanga zinamafanikio japo nazo ni siasa

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV