May 3, 2016Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kusogeza mbele uchaguzi mkuu wa Yanga uliokuwa umepangwa kufanyika Juni 5, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya TFF, Aloyce Komba, amesema uchaguzi huo umesogezwa mbele hadi Juni 25, mwaka huu.

Awali, Yanga ililalamika ikidai uchaguzi huo usogezwe ili wapate nafasi ya kufikiria zaidi mashindano yaliyo mbele yao ambayo ni ubingwa wa Ligi Kuu Bara wanaouwania, fainali ya Kombe la FA  na michuano ya Kombe la Shirikisho. Hata hivyo, mwanzoni TFF iliweka ngumu kuhusiana na madai ya Yanga.

“Tumeyafanyia kazi maombi ya Yanga na kamati ilikutana, tukajadiliana na kuamua kusogeza mbele ili kuipa nafasi Yanga kwenye mashindano ya ligi kuu, fainali ya Kombe la FA na Kombe la Shirikisho.

“Wakati wanajiandaa kumalizia ligi pia wawe wanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi ili visiwepo tena visingizio vingine mbeleni. Muda tuliowapa unawatosha kabisa,” alisema Aloyce.

Hata hivyo, tamko la Aloyce linapingana na kauli aliyowahi kuisema kuwa hawatabadilisha chochote kuhusiana na uchaguzi, hali ambayo inaonyesha wamezidiwa nguvu na hoja za Yanga.   

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV