May 3, 2016


Afeni Shakur ambaye ni mama mzazi wa mwanamuziki aliyetamba katika muziki wa Hip Hop, amefariki dunia kutokana na kukumbwa na shambulizi la moyo, juzi Jumatatu.
 
Taarifa zinaeleza kuwa mama huyo amepoteza maisha wakati akiwa katika Hospitali ya Marin County Sheriff alikokimbizwa baada ya kukutwa na tatizo hilo.

Mama huyo alipata mshtuko huo saa 3:43 usiku wa Jumatatu na alikimbizwa hospitali ambapo ilitangazwa kuwa amefariki dunia saa 4:28 usiku huohuo.

Mpaka mauti yanamkuta akiwa na umri wa miaka 69, Afeni alikuwa mwanzilishi wa Taasisi ya Tupac Amaru Shakur iliyoanzishwa baada ya kifo cha mwanaye huyo ambaye alipata umaarufu mkubwa katika Hip Hop.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV