Bosi wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amezidiwa ujanja na mmoja wa vibaka baada ya kumuibia simu yake ya mkononi anayoitumia.
Tukio hilo lilitokea juzi Alhamisi majira ya saa tano asubuhi kwenye Makao Makuu ya Yanga yaliyopo katika makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.
Muro ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro amesema tukio hilo la kuibiwa simu yake lilitokea kwenye ofisi yake baada ya mtu asiyefahamika kuingia na kuichukua.
Muro alisema, tukio hilo la kuibiwa simu hiyo lilitokea wakati anaandaa taarifa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya kuwapatia waandishi wa habari mara baada ya mkutano na waandishi hao kumalizika.
“Aisee siioni simu yangu moja ya mkononi ya Airtel ambayo ninaitumiga kila wakati, nakumbuka mara ya mwisho niliiacha ofisini kwangu, lakini wakati niliporudi kuichukua sikuikuta.
“Nafikiri hiyo simu itakuwa ndiyo basi imeshaibiwa, hilo tukio la kuibiwa ni la muda mfupi mno, wakati ninatoka ofisini kwangu kwa ajili ya kuandaa ‘Press Release’ kwa ajili yenu waandishi,” alisema Muro.
0 COMMENTS:
Post a Comment