May 9, 2016 Kwa mara nyingine, Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezikumbusha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kuwa mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza tangu Mei 5, 2016.

Bodi ya Ligi kwa sasa inakaribisha maoni, mapendekezo, marekebisho kutoka klabu ili kuboresha uendeshaji wa ligi. Maoni hayo yanapokelewa kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za bodi au kwa njia ya barua pepe tplb.tplb@yahoo.com. Mwisho wa kupokea maoni hayo ni Mei 19, 2016.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV