May 10, 2016

MPIRA UMEKWISHAAAA
-Pamoja na kuwa wamefunga, Mbeya City wanaonekana kutetemeka na kupoteza mpira kila mara
-Kwa hali ilivyo, Yanga wanaonekana kupoza presha, wakitaka kumaliza mechi kwa mabao hayo waliyonayo
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 88, Ngoma anapokea pasi nzuri ya Tambwe, lakini anatumbua shuti kuuuubwaaaaa
GOOOOOOOOO Dk 85 Tambwe shuti kali kabisa na kuiandikia Yanga bao la pili akimuacha Kaseja anazubaaa tu

SUB Dk 84 Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke
DK 82 John Kabanda anapiga krosi nzuri, Salvatory Nkulula  anaunganisha mpira vizuri kabisa lakini unatoka pembeni kidogo nje ya lango la Yanga

Dk 80, Ngoma anaingia vizuri tena, anatoa krosi nzuri kwa Kaseke lakini anashindwa kuunganisha hapa....
SUB Dk 79 Ditram Nchimbi anaingia kuchukua nafasi ya Maundi upande wa Mbeya City
Dk 77 Ngoma anaangushwa tena baada ya kuwachambua mabeki wa Mbeya City, mwamuzi anaonya
Dk 75, Mohammed anaanguka mwenyewe akiwa karibu kabisa na lango la Yanga
Dk 74, Ngoma anawatoka mabeki wawili wa Mbeya City, anampa Kamusoko lakini mpira unaokolewa

Dk 70, Mwasapili anapiga shuti kali mpira wa adhabu, kipa Barthez anadaka vizuri kabisa
SUB Dk 69, Raphael Alpha anaingia kuchukua nafasi ya Redondo upande wa Mbeya City
SUB Dk 66 Mangoma anatoka anaingia Hamidu Mohammed kwa upande wa Mbeya City
Dk 61, Tambwe anaingia vizuri, lakini anawahi vizuri Kaseja
DK 59, Ngoma anaingia vizuri kabisa, yeye na kipa Kaseja, anapiga njeeeeeee
Dk 57, Kaseke anakuwa mchoyo na kupoteza nafasi nzuri. Kama angempa Tambwe, wangeweza kupata bao

Dk 53 hadi 54, Yanga bado wanaonekana kumiliki mpira vizuri hasa eneo la katikati
Dk 50, Msuva anaingia vizuri na kupiga shuti kali kabisa. Lakini Kaseja anaokoa kwa umakini mkubwa. Hata hivyo, mwamuzi anasema waliotea
Dk 47 hadi 49, Yanga wanaonekana kuumiliki zaidi mpira wakigongeana vizuri
Dk 46, Yanga ndiyo wanaanza kwa kasi, lakini mpira unaishia mikononi mwa Kaseja. Mbeya City wanajibu, Barthez anadaka kwa ulaini kabisa

MAPUMZIKODAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 42 hadi 44, mpira unazimama inaonekana kama mashabiki wanafanya vurugu na wachezaji Mbeya City wanajaribu kuwatuliza
Dk 40, Mangoma anapiga shuti kali kabisa akiwa ndani ya 18, Barthez anaokoa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara kwa Yanga
DK 37, Kaseke anaingia kupiga shuti, linazuiliwa na kuwa kona. Anaichonga Msuva lakini Redondo anaondosha
DK 35, Krosi nzuri ya Mwasapili, Barthez anacheza vizuri kabisa
Dk 31, Redondo anajaribu kupiga shuti, hata hivyo linaonekana ni dhaifu, goal kick
SUB Dk 30, Yondani anaingia kuchukua nafasi ya Bossou aliyeumia

Dk 28, krosi safi ya Msuva, Ngoma anaipisha lakini Kaseke anapaishaa buuuuu
Dk 25, Bossou anagongana na mchezaji wa City, yuko chini anatibiwa na watu wa huduma ya kwanza wanaingia na kumtoa. Huenda akabadilishwa
Dk 24, mpira wa adhabu wa Abdul, unatua kichwani mwa Ngoma, lakini Kaseja anaonyesha umahiri na kudaka vizuri kabisa. Anautema, lakini anauwahi ingawa inaonekana mguu wa Tambwe ulitua mkononi mwake

Dk 20 hadi 22, Mbeya City wanaonekana kumiliki mpira zaidi katikati ya uwanja
Dk 18 John Kabanda anaingia vizuri na kupiga krosi safi kabisa, lakini Barthez anadaka kwa ulaini
GOOOOOOO Dk 15, Bossou anaunganisha mpira wa kichwa wa krosi ya Abdul na kuandika bao kwa Yanga
SUB Dk 8, Telela anaingia kuchukua nafasi ya Twite aliyeumia
Dk 5 Twite anatolewa nje baada ya kuanguka. Anatibiwa ingawa dalili zinaonyesha huenda akabadilishwa 
Dk 3, Juma Abdul anaachia shuti kali la mpira wa adhabu, Kaseja anadaka, unamtoka lakini anadaka tena

Dk 2, Chombo anajaribu kuachia mkwaju lakini hata hivyo hakulenga lango
Dk 1, mechi imeanza taratibu huku ikionekana kila timu inaosoma nyingine


KIKOSI
1.Juma Kaseja 
2. John Kabanda 
3. Hassan Mwasapili 
4. Tumba Lui 
5. Haruna Shamte 
6. Kenny Ally 
7. Seleman Mangoma 
8. Ramadhan Chombo 'Redondo'
9. Salvatory Nkulula 
10.Geoffrey Mlawa 
11.Joseph Mahundi


AKIBA:
Hanningtony Kalyesubula 
Hamidu Mohamed
John Jerome
Ditram Nchimbi
Yohana Moriss
Raphael Daud 


Haruna Moshi 'Boban'.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV