May 4, 2016




Real Madrid imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Mei 28 jijini Milan, Italia.

Madrid imetinga fainali baada ya kuitwanga Man City kwa bao 1-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.

Bao la Madrid limepatikana baada ya shuti la Gareth Bale aliyekuwa akipiga krosi kumgonga Fernando na kujaa wavuni.

Pamoja na Madrid kutinga fainali, maana yake Kocha Zinedine Zidane ameandika rekodi yake ya kwanza kucheza fainali hiyo, safari hii akiwa kocha. Lakini Man City imeishia nusu fainali iliyokuwa ni mara ya kwanza kwake kuingia.


Ushindi huo wa bao 1-0, unaipitisha Madrid hadi fainali baada ya sare ya bila bao katika mechi ya kwanza jijini Manchester.











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic