May 11, 2016

MAJIMAJI 0-0 SIMBA FULL TIME 

Dakika ya 90+2: Mchezo umemalizika, timu zote zimetoka nguvu sawa.

Dakika ya 90+1: Majimaji wanashindwa kutumia nafasi ya wazi waliyopata baada ya kufanya shambulizi kali.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba ameonyesha dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 88: Baadhi ya mashabiki wameanza kutoka uwanjani, matokeo bado 0-0.  

Dakika ya 82: Majimaji wanajaribu kushambulia lango la Simba lakini mabeki wa Simba wanakuwa imara kuwazuia.
 
Dakika ya 77: Mchezo bado, haina kasi sana.

Dakika ya 71: Banda ameinuka na mchezo umeendelea, Simba wamepiga faulo lakini haikuzaa matunda.

Dakika ya 69: Abdi Banda yupo chini anachezewa faulo.

Dakika ya 65: Majabvi anashindwa kutumia nafasi anayopata na mpira unakuwa goal kick.

Dakika ya 61: Simba wanashindwa kutengeneza nafasi nyingi, badala yake mchezo unakuwa unachezwa katikati ya uwanja muda mwingi.

Dakika ya 57: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mwalyanzi anaingia Majabvi.

Dakika ya 55: Mchezo bado hauna kasi ya maana, zaidi timu zinapeana zamu kumiliki mpira na hakuna ufundi mwingi.

Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.

Mapumziko 

Dakika 45 zimekamilika. Matokeo bado ni 0-0 hapa kwenye Uwanja wa Majimaji.

Dakika ya 43: Mashabiki ni wengi, Simba bado haijatulia.
 

Dakika ya 41: Kasi ya mchezo imepungua, timu zote zinacheza soka la tararibu. 

Katika dakika za mwanzo, mabeki wa Simba walikuwa wakifanya makosa mengi labda kutokana na kutocheza pamoja mechi nyingi.

Dakika ya 35: Simba wanafanya mashambulizi, Ndemla anapiga shuti lakini kipa wa Majimaji anadaka.


Dakika 30: Matokeo bado ni 0-0, mchezo umekuwa ni wa kubalansi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.


Kikosi cha Simba
1.Peter Manyika
2. Hassan Isihaka
3. Mohammed Hussein ‘Tshabalala’
4. Mohammed Fakhi
5. Novaty Lufunga
6. Abdi Banda
7. Said Issa
8. Said Ndemla
9. Mussa Mgosi
10. Mohammed Mussa
11. Peter Mwalyanzi.

Kocha Jackson Mayanja amerejea kwenye benchi baada ya kumaliza adhabu yake ya kukosa mechi mbili ambazo ni dhidi ya Azam na Mwadui. Mayanja alitolewa uwanjani kwenye mchezo wao dhidi ya Toto Africans.


Simba imefanya mabadiliko ya kikosi kwa asilimia kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV