May 4, 2016Kuna makala inasambazwa kwenye makundi mbalimbali ya Facebook na Whatsapp ukiwa na kichwa cha habari "WALAKA KWA TEAM AVEVA, KUTOKA KWA TEAM MO." 

Makala inazingumzia mambo mengi kuhusiana na uongozi wa Simba na maneno ya kuwakashifu wanachama wa Simba.

Ukisoma juu inaonekana ni makala iliyoandikwa na Saleh Ally kwa kushirikiana na Shaffih Dauda.

Napenda kuwaeleza wasomaji wanaomsoma Saleh Ally kokote kule kuwa makala unayoiona ni upuuzi mtupu kutoka kwa mtu mjinga aliyeshindwa kuwasilisha maoni yake na kuamua kutumia jina langu huku akijua ana jina lake.

Huu ni ujinga mtupu ambao ninaamini hautajitokeza tena. Pia nishauri kwa aliyeiandika kwamba ni vizuri angeonyesha ni mtu anayejiamini kwa kuweka jina lake kwa lengo la kufikisha anachoamini ni sahihi.

Hii ni nchi yenye nafasi ya maoni kwa aliyenayo, kawaida nikiamua kuandika kitu changu, nakuwa huru kufanya hivyo bila ya kificho wala woga. Ninaamini mwandishi huyo aliyesahau jina lake, pia alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo lakini ameshindwa kujitambua na siamini kama anaweza akatengeneza hoja za msingi akiwa muoga au muongo kama alivyofanya. Huo ni unafiki.

Kuandika kitu na kutumia majina ya watu wengine yanaonyesha uoga, uzandiki na unafiki wa hali ya juu unaounda watu wengi wasiojiamini na wasiojielewa. 


Mwisho nimkumbushe aliandika, mimi ni Saleh Ally na si Salehe Ally kama alivyoandika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV