May 3, 2016


Kikosi cha Simba, kinaondoka kesho asubuhi na mapema kwenda mjini Zanzibar kuweka kambi ya siku nne kujiandaa na mechi yao dhidi ya Mwadui FC.

Simba inakwenda Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC inayofundishwa na Jamhuri Kihwelo 'Julio'

Mechi hiyo itachezwa jijini Dar es Salaam, taarifa zinaeleza Simba itaondoka na boti ya asubuhi kwenda Zanzibar.

Pia imeelezwa, Simba inatarajia kurejea Dar es Salaam Jumamosi tayari kabisa kwa mechi hiyo itakayopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV