May 8, 2016


Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi kesho Mei 9, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kuiga timu ya soka ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama jina la Serengeti Boys inayotarajiwa kwenda India Jumatano Mei 11, mwaka huu.

Hafla ya kuiga timu hiyo, itayokahudhuriwa pia na Balozi wa India nchini, Mheshimiwa Sandeep Arya, inatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo mbali ya kutoa nasaha, Dioniz Malinzi ataikabidhi bendera timu ya Serengeti Boys inayokwenda Goa, India kushiriki mashindano maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIFF).


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV