May 8, 2016


Ruvu Shooting leo May 8, 2016, tunaanza rasmi maandalizi ya mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2016/17 utakaoanza mwezi August.

Wachezaji wetu wote, leo wanatakiwa kuripoti kambini baada ya mapumziko mafupi waliyopewa baada ya kumalizika kwa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) tuliyoimaliza kwa mafanikio makubwa tukiongoza kundi B na kuweza kupanda daraja hadi VPL msimu ujao.

Kesho Jumatatu, May 9, 2016 tunatarajia kuanza rasmi kambi ya mazoezi katika eneo letu la 832 Ruvu JKT, uwanja wa Mabatini chini ya kocha Mkuu, Mkenya, Tom Alex Timam Olaba anayesaidiwa na Seleman Mtungwe.

Sanjari na kambi ya mazoezi, tutafanya usajili wa wachezaji kwa nafasi alizoelekeza mwalimu Olaba ambazo ni pamoja na kipa, namba 2, 4, 6, 8, 9 na 10.

Lengo la kufanya usajili huu na kuanza kambi ya mazoezi mapema, ni kukiimarisha kikosi chetu ili kiwe cha ushindani zaidi, msimu ujao wa ligi tuweze kutwaa ubingwa wa soka Tanzania Bara.


Tunakuja sawa na Leicester City ya England. Tuna imani kubwa sana kuyafikia malengo yetu kwani, tunayo dhamira ya dhati kabisa, ndio maana tunaanza kambi mapema. Ombi letu ni HAKI ifanyike kwa kila eneo wakati wote wa ligi, tunaweza, tutakuwa mabingwa kwa uwezo wa kucheza mpira!

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV