May 8, 2016Kocha Mkuu wa MWadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema ana kikosi bora kabisa ambacho hakiwezi kulinganishwa na kile cha Simba.

Mwadui FC watakuwa wageni wa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Julio anasema atashangazwa sana kama wao watapoteza mechi dhidi ya Simba hii leo.

“Kweli mechi itakuwa na ushinda, huenda inaweza ikawa ngumu. Lakini nitashangazwa sana kama nitafungwa na Simba.


“Nasema hivyo kwa kuwa nina kikosi bora kabisa ambacho huwezi ukakilinganisha na Simba. Tunachotakiwa ni kupambana na kushinda na hilo liko wazi,” alisema Julio aliyewahi kuwa beki wa kati wa Simba, kocha msaidizi na kocha mkuu.

1 COMMENTS:

  1. Hana lolote huyo ni Simba damu. Hawezi kuwewekea ngumu kama anavyofanya kwa Yanga.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV