May 4, 2016Kama fasheni fulani hivi. Beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salum Mbonde mkataba wake na timu yake unaisha mwezi huu Ligi Kuu Bara itakapokwisha, amesema timu inayomhitaji impe Sh milioni 20 tu.

Mara mbili huko nyuma ilikuwa katika mipango ya kumsajili Mbonde ili kuimarisha safu yake ya ulinzi lakini mara zote mambo yakashindikana pengine hii inaweza nafasi kwao. 

Baada ya kumkosa Mbonde, Simba iliamua kumsajili Mohammed Fakhi kutoka JKT Ruvu. Yanga nayo iliwahi kumhitaji Mbonde kabla ya kuangukia kwa Vincent Bossou raia wa Togo.

Mbonde amesema mkataba wake unaisha mwishoni mwa ligi na yupo tayari kwenda popote kwa dau hilo la wastani.

Hata hivyo, Mbonde ameweka sharti kwamba dau hilo ni kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele kitakaochomruhusu kuondoka kama atapata timu nyingine nje ya nchi.

Alisema kati ya Juni na Julai, mwaka huu anatarajiwa kwenda kufanya majiribio nchini Tunisia, lakini anaamini ofa hiyo haiwezi kumkataza kusaini kwingine kwani mambo yanaweza yakaenda ndivyo sivyo.


“Mkataba wangu unaisha na kwa timu inayonitaka wanipe Sh milioni 20 tu kwa mkataba wa mwaka mmoja pia waniruhusu kuondoka muda wowote nikipata timu nje ya nchi,” alisema Mbonde.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV