Kocha Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi chake kitakachocheza mechi ya kirafiki leo dhidi ya wenyeji Harambee Stars kwenye Uwanja wa Nyayo Kasarani jijini Nairobi, Kenya, leo.
Katika kikosi hicho, moja ya wageni alioanza nao ni beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ pamoja na Aggrey Morris ambaye anarejea tena Stars akichukua nafasi ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye ametangaza kustaafu siku chache baada ya kudai kuonyeshwa dharau na Mkwasa.
Erasto Nyoni, naye analazimika kucheza katikati kwa kuwa Mkwasa atamkosa beki Kelvin Yondani.
Kikosi kamili, hiki hapa:
1. Deo Munishi
2. Juma Abdul
3. Mohammed Hussein
4. Aggrey Morris
5. Erasto Nyoni
6. Jonas Mkude
7. Himid Mao
8. Shiza Kichuya
9. Elius Maguri
10. Mwinyi Kazimoto
11. Deus Kaseke
BENCHI:
Aishi Manula
David Mwantika
Farid Mussa
Jeremiah Juma
Ibrahim Ajib
Haji Mwinyi
Mohammed Ibrahim
0 COMMENTS:
Post a Comment