May 7, 2016

Msiba mwingine barani Afrika baada ya kiungo wa timu ya taifa ya Cameroon kuanguka uwanjani na baadaye kupoteza maisha.

Kiungo wa Dinamo Bucharest ya Romania, Patrick Ekeng ,26, amekutwa na umauti wakati akiichezea timu yake katika Ligi Kuu ya Romania.

Ekeng alianguka katika dakika ya 70 katika mechi hiyo kati ya timu yake ya Dinamo dhidi ya Viitorul.
Taarifa zimeeleza alifariki saa mbili baadaye akiwa hospitali.

Shirikisho la Soka la Cameroon limethibitisha kuhusiana na kifo cha kiungo huyo.


Lakini nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon, Stephane Mbia ametupia picha mtandaoni akiwa na Ekeng akieleza kusikitishwa kwake na kumpoteza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV