May 7, 2016

RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI (KUSHOTO) AKIWA NA RAIS WA CAF, ISSA HAYATTOU

Kama Yanga ikifuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, basi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litalipwa dola 15,000 na Shirikisho la Soka Afrika (Caf).

Kiasi hicho ni sawa na Sh milioni 32.1, na Caf inakitoa kwa chama au shirikisho la soka ambako timu inayoshika mkia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inakotokea.

Caf inatoa dola 20,000 sawa na Sh milioni 42.9 kwa shirikisho la soka ambalo timu yake imeshika nafasi ya tatu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo. Pia TFF itapa dola 25,000 (Sh milioni 53.6) kama Yanga ikishika nafasi ya pili hatua ya makundi.


Kama Yanga ikitwaa ubingwa basi TFF italamba dola 35,000 (Sh milioni 75.1) na kama mambo yakiwa mabaya, Yanga ikishika nafasi ya pili baada ya kucheza fainali, TFF itapata dola 30,000 sawa na Sh milioni 64.3.

1 COMMENTS:

  1. Title na habari yenyewe ni vitu tofauti. Mamilioni ya TFF au Yanga?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV