May 5, 2016


Wachezaji wa Leicester City pamoja na bench la ufundi watafaidika kwa kupewa magari aina ya 
Mercedes Benz.

Hii ni baada ya timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England na kuwashangaza wengi ambao waliamini ingekuwa ni timu ya kupambana kuepuka kuteremka daraja.

Mmiliki wa timu timu hiyo aria wa Thailand, Vichai Srivaddhanaprabha ameamua kutoa magari 30 aina ya Mercedes B-Class Electric Drive ambayo yanatumia umeme badala ya mafuta ili kuendesha injini yake.


Magari hayo ya kisasa yatakabidhiwa kwa wachezaji na watu wa bench la ufundi.

Bei ya gari moja aina ya Mercedes B-Class Electric Drive ni pauni 32,670 (zaidi ya Sh million 103).

Kabla ya hapo, milionea Srivaddhanaprabha alishawaahidi wachezaji na benchi la ufundi la Leicester safari ya kwenda kula bata jijini Las Vegas, Marekani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV