Klabu ya Barcelona imekubali ofa nono ya kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike.
Gazeti la kila siku la Diario la nchini Hispania limeandika kuwa mkataba huo mpya kati ya Barcelona na Nike utagharimu pauni million 120 kwa msimu na ndiyo utakuwa mkubwa kuliko mingine.
Mkubwa kwa sasa ni ule kati ya Adidas na Manchester United ambao kwa msimu ni pauni million 75.
Imeelezwa pande hizo mbili zimekubaliana mkataba huo uende hadi mwaka 2026.
MIKATABA MIKUBWA
1) Barcelona - Nike (£120m kwa msimu)
2) Manchester United - Adidas (£75m kwa msimu)
3) Chelsea - Nike (£60m kwa msimu)
4) Bayern Munich - Adidas (£46m kwa msimu)
5) Real Madrid - Adidas (£30m kwa msimu)
6) Arsenal - Puma (£30m kwa msimu)
0 COMMENTS:
Post a Comment