May 21, 2016


Baraza Wazee wa Yanga wameshtukia hujuma ndani ya klabu hiyo, baada ya kugundua kuwepo watu wanaotumika kutaka kuivuruga timu hiyo katika kuelekea uchaguzi mkuu.

Kauli hiyo, imetolewa na wazee wa timu hiyo leo kwenye Makao Makuu ya timu hiyo yaliyopo mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Ibrahim Omary Akilimali amesema wanachama wa timu hiyo hawatakiwi kuyumbishwa na baadhi ya wanachama wanaochukia mafanikio ya mwenyekiti wao Yusuf Manji kutokana na mafanikio wanayoyapata.

Akilimali alisema, baadhi ya wanachama hao wanatumika kumchafua mwenyekiti wao kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuivuruga timu kimakusudi.

“Jana wameona umati mkubwa wa mashabiki waliojitokeza kwenye mapokezi ya timu yetu Uwanja wa Ndege baada vijana wetu kuiwezesha timu yetu kufuzu hatua ya makundi ya nane bora kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

“Baada ya kuona umati huo, leo asubuhi tumeona moja ya magazeti likimuandika vibaya mwenyekiti wetu, sasa walikuwa wapi siku kumuandika vibaya hadi walipoona timu yetu imefuzu hatua ya makundi, hivyo ninawatahadharisha wanachama kuachana na maneno hayo,”alisema Akilimali.

"Tunajua hizi njama za kuona Yanga inafeli, ikifanikiwa inawaumiza baadhi ya watu ambao wanataka kuonekana wao ndio wana mafanikio zaidi.

"Wakati fulani tulikuwa nao hapa Yanga lakino hakukuwa na mafanikio yoyote. Sasa wanaona mafanikio ya Yanga kama yanawaumiza wao. Watuache tuendelee kupambana.

"Kama wataendelea hivi itafikia hatua tutatangaza uadui kati yao na sisi, tutatangaza watu waachane kabisa na bidhaa zao."

Hata hivyo, mzee Akilimali hakutaka kutaja jina la mhusika anayewashambulia.

.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic