May 4, 2016


Mechi za mikoani yaani nje ya Dar es Salaam ni ngumu kwa Donald Ngoma wa Yanga, akidai huwa anakamiwa sana na wapinzani huku mabeki wakitumia nguvu nyingi kumzuia.

Ngoma, raia wa Zimbabwe, aliyeifungia Yanga mabao 14, alisema kutokana na hali hiyo, ndiyo maana timu yake imekuwa ikipata ushindi mwembamba kila inapocheza nje ya Dar es Salaam.

Jana Ngoma alitarajia kuichezea Yanga dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. 

Ngoma alisema kucheza ugenini hasa mikoani ni ngumu kuchukua pointi tatu kwa maana timu nyingi za huko zimekuwa zikiwakamia kupita kiasi. 

“Hakuna mchezo wowote rahisi huku mikoani kwa kuwa wenyeji wamekuwa wakicheza kwa nguvu kuhakikisha wanazibakiza pointi katika uwanja wao na wanapocheza na sisi ndiyo wanaongeza umakini.


“Lakini hilo hatuwezi kulitilia maanani sana, kikubwa ambacho tunafikiria ni kuipa timu ubingwa, hivyo tutapambana kwa namna yoyote ile hata kama tukitakiwa tutumie nguvu zetu za ziada itatubidi tufanye hivyo,” alisema Ngoma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV