May 23, 2016


Kazi safi iliyofanywa na benchi la ufundi la Yanga, imeonekana kuwakuna viongozi wa timu hiyo na kuvutiwa kuendelea na makocha hao akiwemo kocha wa makipa, Juma Pondamali aliyemaliza mkataba wake klabuni hapo hivi karibuni.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, amesema benchi lao la ufundi limefanya vizuri na hata wakiliweka suala hilo mezani, watalifikiria pia katika uwiano wa juu katika kuendelea nao msimu ujao.

Ukiachana na Pondamali, pia Kocha Mkuu wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm, naye anamaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu.

“Nisingependa sana kulizungumzia hili, lakini ieleweke kuwa Yanga tuna taratibu zetu katika haya mambo lakini ukipimia uwiano, benchi la ufundi limefanya kazi nzuri sana, kwa hiyo kama kutakuwa na lolote la kufikiria basi litakuwa zaidi ya asilimia 50 tunaweza kuendelea nao,” alisema Sanga.

Ukiachana na Yanga kuchukua ubingwa mara ya pili mfululizo ikiwa chini ya Pluijm, lakini pia wiki iliyopita ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ikiwa ni mara ya kwanza kwa Yanga tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1998 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic