KLABU ya Yanga inadaiwa kuwa imemuacha mchezaji wake Juma Makapu ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa kipindi kirefu. Makapu amekuwa na kikosi cha Yanga kwa kipindi kirefu lakini ameshindwa kabisa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza. Inadaiwa kuwa Makapu anaweza kujiunga na klabu ya Mtibwa Sugar muda wowote kuanzia sasa.
Katika makocha wote ambao wamepita katika klabu ya Yanga hakuna kocha hata mmoja ambaye aliweza kumuamini Makapu na kumpa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
Makapu amekuwa mvumilivu kwa kiasi kikubwa licha ya kukosa nafasi, kama ataweza kwenda Mtibwa itakuwa ni chaguo sahihi kwake kwani atapata nafasi ya kucheza na kuonesha uwezo wake alionao.
Katika vilabu vya Simba na Yanga maisha ya wachezaji wa ndani yamekuwa magumu wachezaji wa kigeni wameweza kutawala kwa kiasi kikubwa. Ukiangalia wachezaji wengi ambao wanakosa nafasi ya kucheza katika klabu ya Yanga pamoja na Simba ni wachezaji wazawa na hii imekuwa changamoto kubwa kwao. Lakini ni jitihada binafsi inabidi ziongezwe na wachezaji wenyewe ili waweze kupata nafasi ya kucheza.
Makapu ni moja ya mchezaji mzuri na mwenye faida ndani ya timu kwani anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja kwahiyo kwenda Mtibwa kunaweza kumsaidia kuonesha uwezo wake na baadae kurudi katika klabu kubwa. Makapu alisajiliwa na Yanga akitokea Zanzibar na ameweza kucheza katika kikosi cha Yanga kwa uaminifu mkubwa.
Kuna mifano ya wachezaji wengi ambao walishindwa kufanya vizuri baada ya kusajiliwa na klabu kubwa. Yanga iliweza kumsajili Rafael Daudi msimu misimu miwili iliyopita lakini alindwa kufanya vizuri, presha katika klabu kubwa imekuwa changamoto kwa wachezaji wengi hasa wazawa na imekuwa ikawafanya kushindwa kucheza mpira vizuri.
Mchezaji kama Hassan Dilunga alishindwa kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Yanga aliweza kwenda Mtibwa na baadae akasajiliwa tena na klabu ya Simba, kwahiyo kukubali kurudi kuanzia chini sio jambo baya katika maisha ya soka wapo wachezaji wengi wakubwa duniani waliweza kufanya ivyo na leo wanachezea vilabu vikubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment