May 30, 2016Vikundi sita kati ya 12 vilivyoshiriki mashindano ya Ngoma za Asili katika Tamasha la Majimaji Selebuka linaloendelea mjini Songea, vimejikita kusifia utawala wa awamu ya tano chini ya Dk John Pombe Magufuli, kama chambo ya kujinyakulia ushindi nafasi ya kwanza.

RAIS MAGUFULI
Tamasha hilo linaloendelea kwenye Uwanja wa Makumbusho ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji mjini Songea, jana liliingia katika siku ya pili ambapo jana ilikuwa ni zamu ya mashindano ya ngoma za asili ambazo mshindi anatarajiwa kupatikana leo Jumatatu.


Vikundi vya Boma Jaribu, Mganda Kilagano, Matogolo, Kioda Mji Mwema, Mganda Mshindo na Boma Kilagano vilijikuta vikigonganisha nyimbo, zote zenye ujumbe wa kusifu uongozi wa Dk Magufuli kwa jinsi anavyokula sahani moja na mafisadi, watumishi hewa na kutetea haki za wanyonge.


Mashindano hayo yaligawanywa katika vipengele vitatu; Ngoma ya Kioda, Ngoma ya Mganda na Mchanganyiko. Mshindi kwa kila kipengele atajinyakulia laki tatu, laki mbili kwa mshindi wa pili na laki moja kwa mshindi wa tatu. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV