May 30, 2016Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ameshtukia dili mapema na kuamua kuwaomba viongozi wampatie video za mechi za wapinzani wao kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, hasa TP Mazembe.

Yanga imepangwa Kundi A ikiwa na timu za MO Bejaia (Algeria), Medeama (Ghana) na TP Mazembe huku Kundi B, likiwa na Kawkab (Morocco), Etoile du Sahel (Tunisia), FUS Rabat na Ahly Tripoli (Libya).

“Ninahitaji muda zaidi wa kuwaangalia TP Mazembe kwenye baadhi ya mechi za mwisho walizocheza kwa ajili ya kuwaona wachezaji wenye madhara nitakaotakiwa kuwadhibiti mara tutakapokutana nao.

“Ninaamini hao Mazembe sidhani kama ni wale niliowaona nikiwa naifundisha Berrekum Chelsea ya Ghana, hivyo ninahitaji muda zaidi kwa ajili ya kuwaangalia,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV