May 18, 2016

HALL
Kocha Stewart John Hall, sasa si kocha wa Azam FC tena.

Hall raia wa Uingereza amekaa meza moja na Azam FC, wamekubaliana na amebwaga manyanga, anaondoka zake.

Uongozi wa Azam FC, umethibitisha kwamba Hall si kocha wao tena baada ya kumalizana naye.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema: "Kikosi sasa kitabaki chini ya kocha msaidizi, Dennis Kitambi na ndiye atamalizana nayo ligi pamoja na mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga.

“Tumekaa pamoja na kukubaliana pande zote mbili, alituomba kuachia ngazi kwa lengo la kutafuta changamoto nyingine nje ya nchi.

“Tunamtakia kila la kheri aendako, pia tunamshukuru kwa mafanikio kwani tuko nafasi ya pili katika ligi na pia fainali ya Kombe la FA."

REKODI ZA HALL:
MECHI       62
SHINDA     41
SARE         16
POTEZA      5
Hii ni tokea alipotua Azam FC Juni, 2015.
MABAO YA KUFUNGA  111
MABAO YA KUFUNGWA  41
BILA KUFUNGWA (Mechi 31)

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV