May 18, 2016

MATEJA BAADA YA KUTUA KATIKA MJI WA DUNDO NCHINI ANGOLA

Mwandishi wa gazeti la Michezo na Burudani la Championi, Musa Mateja amezuiwa kuitumia kamera yake kupata picha katika mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya wenyeji Sagrada Esperanca dhidi ya Yanga.

Mateja ambaye hadi sasa ni mwandishi pekee aliyesafiri na Yanga, amezuiwa na viongozi wa Esperanca, jambo ambalo limezua mzozo mkubwa mjini Dundo.

Yanga ipo Dundo, Angola kuwavaa Esperanca katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho. Mechi ya kwanza jijini Dar, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.

Mateja alitangaziwa uamuzi huo na viongozi wa Esperanca baada ya kumuona anapiga picha za mazoezi pekee ya Yanga kabla ya mechi ya leo.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga aliingilia hilo na kuwasisitiza Mateja ana haki ya kupiga picha mnato.

YANGA WAKIWA MAZOEZI JANA JIONI, HAYO NDIYO MAZOEZI PEKEE WALIYOFANYA

Sanga aliwaeleza kwamba hata shirikisho la soka nchini humo limewaruhusu isipokuwa picha za video.

Alipotaka kujua sababu, Mateja alielezwa eti waandishi wa Angola walipokutua nchini wakiwa na Sagrada na pale awali walipokuja na Recreativo Libolo, hawakupewa ushirikiano. Jambo ambalo si kweli hata kidogo.

Tayari Yanga wameweka tahadhari kwa kuwa kitendo hicho kutaka kumzuia kupiga picha wakati mechi inaendelea, kinaonekana ni maandalizi ya “kuiminya Yanga” katika mechi hiyo.

Inaonekana Esperanca wamepanga kufanya fitna badala ya soka, hivyo hawataki kuona waandishi wakifanya kazi yao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV