May 2, 2016


Na Saleh Ally
SARE ya bao 0-0 kati ya Simba dhidi ya Azam FC, sasa nui uthibitisho kwamba nafasi ya ubingwa kwa Yanga ni asilimia 95.

Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa pointi 62, inafuatiwa na Azam FC yenye 59 na Simba 58, baada ya mechi ya jana.

Iwapo Yanga itashinda mechi zake tano zilizobaki, itafikisha pointi 77. Azam FC ikishinda zote itakuwa na 71 na Simba itakuwa na 70.

Ukiangalia mwendo huu, lazima ukubali kwamba Simba kuzungumzia ubingwa leo, zaidi ni suala la miujiza tu. Badala ya kutegemea ishinde iwe bingwa italazimika kutegemea mawili. Kwanza ishinde mechi zote na kuomba dua kwa Yanga ipoteze mechi angalau tatu katika tano.

Lakini wakati Simba itakapokuwa inaomba dua mbaya kwa Yanga, bado italazimika kuomba dua mbaya kwa Azam FC nayo ipoteze angalau mechi moja na yenyewe ishinde zote.

Nafikiri unaweza kufananisha kama ule mchezo unaoendelea kwenye La Liga kati ya Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid ingawa wao wana pengo dogo la pointi kwani ni pointi moja pekee.

Mara baada ya mchezo wa jana, nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema hawataka tamaa, wataendelea kupambana hadi mwisho ili wajue wamekosa au wamepata.

Kwangu nampongeza, kama nahodha lazima aseme hivyo kuendelea kuiweka juu morali ya timu. Lakini ukweli utaendelea kuwabana Simba kwamba wanalazimika kushinda hadi mwisho na hilo ni jukumu lao, lakini Azam aharibu, Yanga naye aharibu, acha tungoje miujiza ya soka na kama ingekuwa maoni yangu binafsi, ningesema sasa Simba wacheze kwa heshima, nafasi ya ubingwa kwao ni asilimia 25 tu.

Hilo la ubingwa, nawaachia Simba na wanaoshindana. Mkude na kikosi chao wanaopambana pia. Lakini mimi nazungumza na viongozi wa Simba sasa.

Kwamba wakati umefika wabadilike na kuachana na hisia za kuifanya Simba timu bora katika ukuzaji wa vipaji badala ya kuangalia mioyo ya mashabiki na wapenzi wao ambao wangependa kuiona timu yao inabeba makombe au kucheza michuano ya kimataifa.

Inawezekana kweli kumekuwa na hujuma ndani ya soka, kwamba kuna taarifa za michezo michafu. Lakini tujiulize, kweli hizo hujuma zinaitafuna Simba pekee, wengine hapana?

Kama hiyo haitoshi, bado unaweza kujiuliza katika hali ya kawaida. Ukaangalia usajili wa Yanga na ule wa Azam FC, utanieleza baadaye unaona upi unaonyesha watu wako makini na kweli wana kikosi cha kubeba makombe.

Bado, Simba wanapaswa kubadili mfumo sasa. Vijana ni jambo zuri kuwa nao, lakini soka ni biashara inayotakiwa kumaliza. Wenyewe uwezo wa kumaliza biashara hiyo ni wachezaji wazoefu.

Vipaji katika michezo ni jambo bora, lakini kuwa na wachezaji wenye uzoefu wanaojiamini, wenye uwezo wa kubadili matokeo pia ni jambo jema.

Hiki ni kipindi sahihi ambacho Simba badala kuweka nguvu nyingi kuhakikisha wanataka kuwa mabingwa. Mimi ningewashauri nguvu hizo wazitumie kuanza kujenga kikosi bora wakianza na wachezaji kutoka ndani ya Tanzania kabla ya kwenda nje kwa kuwa wanawajua waliowaangusha na wanapaswa kutoka, pia wanawajua walio nje ya Simba wanaoweza kuwasaidia ili wabanduke kutoka walipo. Misimu minne bila ya kucheza michuano ya kimataifa ni aibu asee!



3 COMMENTS:

  1. Yanga wana kikosi bora zaidi, imeweza kuzifunga karibu timu zote 14 zinazoshiriki ligikuu ya Vodacom 2015/16 ukiacha Azam,ambayo kidogo ni ya kimataifa kama Yanga.Katika timu hizo 14 baadhi kama vile Simba zimechezea vichapo mara mbili nyumbani na ugenini

    ReplyDelete
  2. Hebu tafakarini hizi kauli.
    -YANGA..Tunataka kutetea ubingwa.
    -AZAM..Tunataka ubingwa mwaka huu.
    -SIMBA.. Ubingwa kwetu ni lazima mwaka huu.

    ReplyDelete
  3. Kama Simba imesajili wachezaji wa kigeni 7 na wanacheza wote bado unasema wanajenga timu?Mbona mnataka kuigeuza nyeupe kuwa njano?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic