May 19, 2016Simba wamekubaliana kuangalia wachezaji wenye uwezo mkubwa na kupunguza idadi kubwa ya vijana katika kikosi chao.

Uamuzi huo unatokana na Simba kuona inaporomoka kwa kiasi kikubwa licha ya kutoa nafasi kubwa kwa wachezaji vijana.

Uamuzi huo wa Simba, unafuatia kipindi kigumu cha misimu minne ya kutoshiriki michuano ya kimataifa.

“Si kwamba kikosi hakitakuwa na vijana, lakini kuna haja ya kusajili wachezaji ambao ni kwa ajili ya kuchukua kombe,” kilieleza chanzo.

“Tunajua Wanasimba wamechoka, tuliwaamini sana vijana na kweli tulikuwa na nafasi ya kuchukua kombe. Lakini kwa jinsi mambo yanavyokwenda tunaona kama inazidi kuwa si hali nzuri.

“Acha tufanye na hiki ambacho tunataka kukiamini, baada ya hapo tutajua mbele. Tunajua hapa kinachotakiwa ni kufanikiwa na kupiga hatua kutoka hapa tulipo.”


Tayari kuna kila dalili Simba itaachana na wachezaji wake wa kigeni kwa asilimia 90 na kipa Vicent Agbani ndiye anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kubaki. Mwingine alikuwa ni Justuce Majabvi lakini inaelezwa ameomba kuondoka kwa kuwa mkewe amepata kazi nchini Australia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV