May 27, 2016

JUMA ABDUL

Wakati Simba ikiwa katika harakati za kutaka kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara imejikuta ikigonga mwamba kwa mara nyingine tena Yanga baada ya kushindwa kumnasa beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul.

Simba walitaka kulipa kisasi kwa kutaka kumsajili Abdul baada ya Yanga kumchukua Hassan Kessy, lakini dili lao likagonga mwamba.

Abdul ambaye sasa yupo katika kiwango cha juu mkataba wake na Yanga ulitarajia kufikia tamati hivi karibuni lakini baada ya uongozi wa klabu hiyo kusoma alama za nyakati na kuona kuwa unaweza kumpoteza ulifanya naye mazungumzo na kumwongezea mwingine wa miaka miwili kimyakimya.

Habari za ndani zinaeleza zimedai kuwa  baada ya Simba kuondokewa na Kessy ilipata taarifa kuwa Abdul naye mkataba wake unamalizika hivi karibuni hivyo ni vizuri ikafanya naye mazungumzo ili iweze kumsajili.

“Walimfuata Abdul na kuzungumza naye kisha wakamwambia kuwa wapo tayari kumpatia Sh milioni 60 ili aweze kujiunga na timu yao.

“Hata hivyo, Abdul aliwambia kuwa wamechelewa kidogo kwani tayari alikuwa ameshamalizana na Yanga hivyo hawezi kusajili tena Simba, jambo ambalo liliwauma sana viongozi hao,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Abdul ambaye ni beki bora wa pembeni kwa sasa alisema: “Ni kweli wanifuata lakini kwa sasa sipo tayari kuondoka Yanga."

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic