May 18, 2016

MAZINGIRA YA UWANJA HUO YALIVYO SASA. MECHI ITAANZA SAA 11 KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI
Esperanca wanaonekana kupania kuwadhulumu waandishi wa habari haki ya kuripoti baada ya kumpokonya kamera mwandishi Musa Mateja kwa madai haruhusiwi kuingia uwanjani wakati timu yao inapambana na Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Mateja ametolewa nje kwa madai hatakiwi kupiga picha na huo uamuzi umepitishwa na uongozi wa klabu hiyo.

Mwandishi huyo aliambiwa tokea jana kuhusiana na hilo, lakini Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga aliwaeleza kwamba shirikisho la soka la nchi hiyo liliwaambia picha za video pekee ndiyo hawatakiwi kuchukua.

Lakini leo inaonekana mwandishi huyo anaonekana anaweza akaripoti kuhusiana na figisu zao, wametaka aondolewe.

Taarifa zilizoingia hivi punde zinaeleza tayari Sanga yuko eneo la tukio, pia kuna mwandishi wa Mwanaspoti, Gift Macha naye amezuiwa kuingia kama ilivyo kwa Mateja.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV