May 7, 2016


Kikosi cha Sagrada Esperanca ya Angola kiliwasili nchini usiku wa kuamkia jana huku kikiweka masharti kadhaa lakini kali zaidi ni kukataa hoteli waliyokubali kufikia mwanzo.


Maofisa wa Esperanca baada ya kuwasili nchini walikodisha basi la Kichina lenye namba za usajili T 347 DCF ambalo lilitumiwa pia na Al Ahly ilipokuja kucheza na Yanga mwezi uliopita.


Hali ya sintofahamu ilitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 6:00 usiku huo ambapo maofisa hao waligoma kutumia hoteli waliyopangiwa na Yanga wakidai haina hadhi.
AHLY WALITUMIA BASI HILO
“Mimi nawashangaa hawa jamaa, mchana tulienda wote kukagua hoteli na wakakubali kila kitu lakini sasa hivi wanasema hawaitaki eti baadhi ya vyumba si vizuri.

“Wamesema kesho watahamia Kilimanjaro (Hyatt Regency) kwani walisikia Al Ahly walifikia hapo, mimi nawaacha waamue wanavyotaka maana hata gari wamekodi lile lililotumiwa na Al Ahly,” alisema Ramadhan Wasso ambaye ni mwenyeji wa Esperanca aliyepangwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Yanga. 


Wasso ambaye ni beki wa zamani wa Yanga na Simba, alisema anashangazwa na mambo mengi yalivyopanguliwa na maofisa wa Esperanca wakati awali walikubaliana.

Maofisa wa Esperanca waliokuwepo uwanjani hapo, hawakuwa tayari kutolea ufafanuzi hali hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV